TAFUTA HAPA

Loading...

MSHINDI WA MWAKA JANA WA SHINDANO LA MWANAMAKUKA BI AZIZA MBOGOLUME AFARIKI DUNIA.

Kikundi Cha Unity Of Women Friends, kupitia mradi wao wa Mwanamakuka Awards na washirika wake, Benki ya wanawake TWB na Cloud Entertainment group. Wana masikitiko makubwa kwa kumpoteza mshindi wa mwaka jana 2013, Bi Aziza Mbogolume.
 Amefariki leo mchana, na anatarajiwa kuzikwa kesho saa tisa mchana nyumbani kwake Magomeni.
Aziza alikuwa mwanamke jasiri, mwenye uthubutu wa kufanya biashara kupitia kipaji chake cha kuchora.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi,amina.

MY HOBBIES...MAUA

Wale mlioulizia stand za maua zinapouzwa piga simu namba hii hapa utawapata 0717004838


 Kwenye maisha haya kila mtu ana vitu anapenda na vinamfurahisha yeye mwenyewe.
Kuna watu wengine wanapenda magari na ni machizi magari kila leo ana jipya.Mie hapa sina intrest kabisa na magari nina forbia kabisa ni vile nifanyeje lazima nilipande linifikishe niendako.
Napenda maua na nacollect maua nikiliona mahali zuri nachanganyikiwa kabisa ninavyoyafurahia.Najua kuna watu wanapenda maua kama mimi na kama haupendi bahati mbaya lakini lazima na wewe kuna kitu chako kingine unapenda.ZAMANI NILISUMBULIWA SANA NA HILI TATIZO.

Siku hizi huku kwenye mitandao watu wana maneno na misemo ambayo wakati mwingine ukifatilia ni kweli tupu.Haya maneno ni kweli kabisa kuna wakati nilikuwa hivyo.Unaweza kuwa una marafiki wewe kichwani kwako unadhani ni watu wako kumbe walaaa.Sasa kwasababu una nia safi nao unajikuta kila siku wewe ndio uwasabahi,uwatafuta na bado wasipatikane yaani watakuwa karibu na wewe kwa sababu ya situation flani inayomuhusu yeye akipita hiyo hali humuoni ng'oo.
Au anakuwa karibu na wewe aliakamilishe kitu flani akikamilisha humuoni unabaki wewe kumtafuta atakupa sababu laki 8 za kwa nini siku hizi humuoni.Kuna watu watakuwa karibu na wewe ili akufanye ngazi ya kupanda mahali flani akishapanda anakutupa kule.Mifano ni mingi sana ambayo hata wewe mdau unaweza kuongezea.Nilipokutana na huo msemo nikasema ngoja niuweke hapa inawezekana kuna mtu mwingine nae haya yanamfika.
i

MSHINDI WA SHINDANO LA SAA KUTOKA MBEYA AKIWA TAYARI KASHAPOKEA ZAWADI YAKE.

Wakati wa michuano ya kombe la dunia niliweka shindano la kubashiri.Nikasema atakae patia nani kushinda kombe la dunia na kwa idadi ya magoli atajishindia saa ya mkononi.Watu wengi walijibu na kama watatu walipatia hivyo kunilazimu kuchagua wa kwanza kabisa kupatia.Anaitwa Getruda Jackson ni mwenyeji wa Mbeya ila kwa sasa yupo Dodoma kikazi.Hongera sana kwa kushinda kama unakumbuka katika fainali za kombe la dunia kati ya ujerumani na Argentina.Ujerumani ilitwaa kombe hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya argentina.Ndivyo Getruda alibashiri.Nitakuwa naweka vishindano vidogo vidogo na kutoa zawadi kwa wasau wangu angalau mara moja kwa mwezi.

MAPISHI YA MABOGA NA VIAZI VITAMU,MBOGA MBOGA NA MINOFU YA KUKU.


MABOGA NA VIAZI VITAMU
Nimechukua maboga nikaamenya nikaosha na kukata kata vipande vidogo vidogo.Na viazivitamu pia nikamenya na kuosha kisha nikakata vipande vidogo vidogo nikavichanganya na maboga kwenye sufuria moja.Nikaweka maji kiasi chumvi kidogo na 
Kisha nikavibandika jikoni vichemke na kuiva kwa muda wa nusu saa.Vilipoiva nikavitoa jikoni nikachuja maji yote nikaviponda ponda na kuwa laini kabisa kisha nikaviweka siagi itokanayo na maziwa.Nikakoroga vizuri ili iyeyuke na viwe bado vya moto na harufu nzuri baada ya hapo ikawa tayari kuliwa.

MBOGA MBOGA
Kwenye mboga mboga kuna kitunguu maji,kitunguu saumu,karoti,hoho nyekundu na njano,maharage machanga,brocol hii mboga sijui kiswahilo chake na kolimaua.
Niliweka mafuta kwenye kikaango natumia mafuta ya alizeti yalipopata moto nikaweka kitunguu nikakaanga pamoja na kitunguu saumu vilipokuwa brown nikaweka nyanya kidogo.Nyanya zilipoanza kuiva nikaweka chumvi na baadae nikaweka mboga mboga zote na kuzikoroga kuchanganya vizuri.Nikaongezea ndimu ili kuichangamsha.Baada ya dk 10 nikaipua maana haitakiwi kuiva sanaa kidogo tu.

KUKU MINOFU
Mnofu wa kuku ni eneo la kidari huwa lina mnofu wa kutosha.Nilichofanya niliosha kuku vizuri nikamkamulia ndimu na nikaweka tangawizi ilotwanga ikalainika vizuri na chumvi.Nikaweka kwenye frying pan kisha motoni nikaongeza maji kidogo.Nikamuacha aive mpaka maji yote niloweka yakauke kabisa na kuku akauke na kujikaanga na mafuta yakr kama yapo.Nikanyunyizia pili pili manga kwa juu akakauka kabisa kisha nikamtoa tayari kwa kuliwa.Hapa sijatumia mafuta kabisa.

Kama sahani inavyoonekana katika picha hapojuu inaliwa huo mchanganyiko wa viazi vitamu na boga,mboga mboga na kuku.Ni tamu mno na rahisi kupika.Hizo mboga mboga unaweza pia kuzila na wali hata chips hiyo kuku.

MY HOBBIES....MAUA

Nilisema ntakuwa nawashirikisha sehemu ya vitu ninavyopenda kufanya.Kila siku kwenye maisha tunashauriwa kuongeza new hobbies kama inawezekana.Kuna kitu nakipenda sana na nikiwa mdogo nilikuwa nakimudu mno,kuchora.Nilikuwa nachora sana nilipoanza maisha ya kazi sijawahi kuchora tena.Nahisi nitarejea tena kwenye kuchora soon nitaanza kama mwanafunzi naona maana sijui tena ila kama ni kipaji ninacho ndani basi kitafufuka tu.
Haya maua niliyapanda mwenyewe kwa mkono wangu na sasa yameshamiri vyema.

DADA DINA CARES NA WATOTO WA KITUO CHA ZAIDIA SINZA


Kwa uwezo wa Mungu tulifanikiwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha Zaidia kilichopo sinza madukani.Kwa michango tulopokea tumefanikiwa kuwapelekea nguo kidogo,unga kg 150,maharage kg 100,mchele kg 100,unga wa ngano kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia ndoo 3,sabuni za miche box 4,mafuta ya kujipaka dozen 4,miswaki na dawa za meno.
Tulikaa na watoto tukacheza kidogo na kuwapa vichangamsha mdomo baadae kurejea makwetu.Shukrani kwa mliochanga chochote ulichobarikiwa maana kutoa ni moyo si utajiri.Kuna matajiri lakini hata sh 10 yake hatoi kwa haya mambo.Kuna mtu unaona kajinyima kweli mpaka kachangia na bado kwa watoto anaenda kuwatembelea.Asante kwa team nilokuwa nayo Easter Nyalusi,Halima Temu,GLoria Shayo,Vivian Mchome,Blandina Mvungi,Ummy Kitwana,Tuntufye Abraham,Kaka Richard Chambai na mwanamuziki Mwasiti alikuja pia kujumuika nasi.Bado tunavituo vitatu Sifa bunju,house of hope mabibo na vetenari temeke ambavyo tutavifikia weekend hii.

JUMAMOSI ILOPITA DADA DINA CARES ILIPOTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA MWANDALIWA.


Tunashukuru Mungu anaendelea kutupigania na yale tunayojadhamiria kuyafanya kwa dhati  yanatimia.Ni mwezi sasa nilipoanza kuchanga hela za kununua vitu hasa chakula na kupeleka kwenye vituo vya watoto yatima.Na jumamosi ilopita tuliwasilisha vitu katika kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kipo mbweni.
Tulipeleka unga kg 150,mchele kg 100,maharage kg 100,sukari kg 50,unga wa ngano kg 50.Pia tulipeleka ndoo 4 za mafuta ya kupikia,box 4 za sabuni za miche za kufulia ambazo kila box inakaa miche 10.Mafuta ya kujipaka dozen 4,dawa za meno box zima,miswaki,malapa n.k
Kama ujuavyo chakula lazima watoto wale kila siku hivyo tunashukuru tumefanikisha hilo.Nawashukuru wote waliojitolea kufanya kazi na mimi hasa Halima Temu,Gloria Shayo,Ummy Kitwana na kijana anaitwa Richard Chambai.Hizi ni kazi za kujitolea hazina malipo yoyote lakini wao walijitoa na tukafanikisha.Nitakuwekea na picha tulipoenda kituo cha Zaidia kilichopo Sinza madukani.

MAISHA

MIMI NA WEWE